Sifa za kujiunga na chuo cha sheria ngazi ya cheti: Je, unatamani kusoma sheria au kuwa Wakili, Hakimu au Jaji? Hongera! Soma vigezo na mlolongo wote hapa chini.
Sifa za kujiunga na chuo cha sheria ngazi ya cheti
(i) : Kwa ngazi ya shahada (degree).
– Ukitaka kusoma degree ya sheria na umehitimu SECONDARY kidato cha sita (6), unatakiwa uwe umefaulu masomo mawili, kiingereza na historia, uwe walau na “D” mbili na kuendelea. Na kama hujasoma na kufaulu History na English A – LEVEL (KIDATO CHA SITA), labda umesoma sayansi (PCM, PCB, CBG n.k) au umesoma History na English A Level lakini hujafikisha alama “D” ya masomo hayo, na unatamani kusoma sheria, basi uwe una credit ya history na kiingereza kule O level, yaani uwe umeyafalu kwa kiwango cha alama “C” na kuendelea kule kidato cha nne (4).
NB: Kwa kuwa sasa Kiswahili ni lugha rasmi ya Mahakama na sheria zote zinatakiwa kuandikwa kwa Kiswahili, HUENDA wanaotaka kusoma sheria wakatakiwa kufaulu na kiswahili.
-Kama unatokea Diploma, uwe na GPA ya 3.0
(ii) Kwa ngazi ya DIPLOMA (stashahada).
– Ukitaka kusoma diploma ya sheria inategemea una elimu gani:
-Kama umemaliza kidato cha sita uwe na cheti cha form six na walau principal pass moja (D), Subsidiary (S) moja na angalau ‘D’ nne (four passes) za kidato cha nne, ila isiwe za masomo ya dini. NB: Somo moja liwe ni somo la kiingereza (English), na
-Au uwe umehitimu certificate ya Sheria (Certificate in Law (NTA Level 4).
(iii) Kwa ngazi ya CHETI.
Ukitaka kusoma certificate ya sheria unatakiwa uwe na cheti cha kidato cha nne na ufaulu wa angalau ‘D” nne, mojawapo iwe ni ya somo la English.
2: Kama una hizo sifa, hatua inayofata ni kutuma maombi kuchagua chuo unachotaka na kwenda kusoma. Utachagua mwenyewe unataka kuanzia cheti (certificate), stashahada (diploma) au shahada (degree). Kulingana na matokeo yako.
Mfano kama umehitimu na kufaulu kidato cha sita, utaenda chuo kikuu kusoma shahada (degree). Kama umefeli au kama marks hazitoshi kwenda chuo kikuu, utaenda kusoma cheti au diploma na baadae utaunganisha hadi degree ukitaka.
Muda wa kusoma inategemea na level uliyopo (unasomea cheti, diploma au degree). Mathalani, certificate ni mwaka mmoja, diploma ni miaka miwili na degree miaka mitatu au minne (inategemea umeenda chuo gani). Ukimaliza hapo umekuwa mwanasheria lakini sio Wakili.
Unawezaje kuwa Wakili? Au Hakimu? Au Jaji? Kwa sababu Mahakimu na Majaji wanachaguliwa kutoka kwenye watu wenye sifa za kuwa Wakili, basi tutajikita kuangalia mchakato wa kuwa Wakili.
MCHAKATO WA KUWA WAKILI.
Sifa na Mchakato wa kuwa Wakili nchini Tanzania (Bara) unapatikana kwenye Sheria ya Mawakili (The Advocates Act) na Sheria ya Shule ya Sheria Tanzania (The Law School of Tanzania Act).
MCHAKATO WA KUWA WAKILI KABLA YA KUANZISHWA KWA SHULE YA SHERIA KWA VITENDO (LAW SCHOOL), 2007.
Kwa sababu Law School imeanzishwa mwaka 2007. Watu waliosoma shahada (degree) ya sheria kabla ya mwaka 2007 walitakiwa kufata utaratibu ufuatao ili kuwa Mawakili.
1: Uwe na shahada ya Sheria (LLB).
2: Kufanya mafunzo (internship) kwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na kwa Wakili wa kujitegemea.
3: Kutuma maombi kwa Jaji Mkuu.
4: Kufanyiwa interview (bar examination) mbele ya Baraza la Elimu ya Sheria / Council of Legal Education (CLE).
5: Kufanyiwa interview mbele ya Jaji Mkuu (Chief Justice).
6: Kuapishwa (admission)
7: Kuandikishwa jina (enrollment) kwenye orodha ya Mawakili (Roll of Advocates).
MCHAKATO WA KUWA WAKILI BAADA YA KUANZISHWA KWA SHULE YA SHERIA KWA VITENDO (LAW SCHOOL), 2007.
Kwanza tufahamu, “Law School ni nini?” Hiki ni Chuo cha Uanasheria kwa vitendo ambacho kinatoa mafunzo yanayolenga kumuandaa mhitimu wa shahada ya kwanza ya sheria (LLB) kufanya kazi ya Uwakili (Uhakimu, Jaji n.k)
Je, ni lazima kwenda Law School? Inategemeana. Lakini jibu la jumla, kama unataka Kuwa Wakili, Hakimu au Jaji wa Mahakama nchini Tanzania, kwenda Law School ni lazima.
Sasa kwa nini nasema inategemeana? Ni akina nani wanaweza kuwa Mawakili au kufanya kazi za Mawakili bila kupita Law School?
Kufatia Marekebisho ya Sheria ya mwaka 2020 (The written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 3), Act 2020) yaliyorekebisha Sheria ya Shule ya Sheria Tanzania (Law School of Tanzania Act), sheria inatoa msamaha kwa baadhi ya wanasheria wenye vigezo maalum, ambao kwa mujibu wa Sheria walipaswa kupititia Law School, lakini kutokana na nafasi zao katika Utumishi wa Umma hawawezi kuhudhuria mafunzo hayo. (Hasa watumishi wa Mahakama na wanasheria kwenye ofisi za umma, unatuma maombi kwa Waziri husika unasamehewa kwenda law school). Soma PART XI section 42 ya amendments.
Lakini, kiujumla, kwa ambao wamehitimu shahada ya sheria baada ya mwaka 2007, wanatakiwa kufata utaratibu ufuatao ili kuwa Wakili.
1: Uwe na shahada ya Sheria (LLB). Soma section 8(1)(a)(i) ya Sheria ya Mawakili na Section 11(1) ya Law School of Tanzania Act.
2: Kuhudhuria mafunzo ya sheria kwa vitendo (Post Graduate Diploma in Legal Practice) katika shule ya sheria kwa Vitendo (Law School). Section 12 ya Law School of Tanzania Act, CAP 425.
See also:
- Kwenda South Afrika sasa ni Bure Kuitazama Yanga SC
- Matokeo Namungo FC vs Kagera Sugar Leo 02 April 2024
- Vilabu tajiri zaidi barani Afrika 2024 – Transfer Market
- Ratiba ya Simba SC mwezi Aprili 2024 NBC
- Waamuzi wa michezo ya Robo Fainali CAF wiki hii
- Bei ya Magari ya MAZDA ATENZA Tanzania 2024
- Sifa za kujiunga na vyuo vya ualimu ngazi ya diploma 2024/2025
- Sifa za Kujiunga na Chuo cha Utalii 2024
- Sifa za Kusoma Civil Engineering 2023/2024
- Sifa za Kujiunga na Kozi ya Information Technology (IT)
- Paul Makonda ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Leave a Reply