Sifa za mashairi ya kimapokeo

Sifa za mashairi ya kimapokeo: Shairi ni aina ya fasihi. Mashairi ni tungo zenye kutumia mapigo ya silabi kwa utaratibu maalumu wa kimuziki kwa kutumia lugha ya mkato, lugha ya picha na tamathali za semi.

Kuna mashairi yanayofuata taratibu za kimapokeo, yaani yanazingatia taratibu za urari na vina, mizani, idadi sawa ya mistari, vituo na beti. Mashairi hayo huwa na mizani 14 au 16 katika kila mstari, yaani mizani 7 au 8 kwa kila kipande cha mstari.

Mashairi ya kimapokeo

Haya ni mashairi yanayozingatia kanuni za muwala/urari (ulinganifu) wa mizani, vina, idadi ya mistari katika kila ubeti na kituo katika shairi. Vilevile huitwa mashairi funge.

Aina ya mashairi kulingana na mtindo huu wa mapokeo,hupatikana kwa kuangalia idadi ya mishororo katika kila ubeti.

Sifa za mashairi ya kimapokeo

Sifa za mashairi ya kimapokeo

  1. Uteuzi wa sauti,silabi au maneno katika shairi ni wa kipekee usiozingatia sarufi.
  2. Mpangilio wa maneno katika mshororo huwekwa kwa utaalam zaidi kulikokatika riwaya.
  3. Uteuzi wa maneno katika shairi zima kwa kawaida huwa na maana maalum na si suala la kuteuwa kiholela holela.
  4. Huwa na matumizi ya jazanda na taswira.
  5. Huwa na matumizi yatamathali za usemi huwa na maana ambazo hujenga maudhui na kuleta mvuto katika shaiti na kufanya kazi za kishairi iwe ya sanaa zaidi
  6. Huwa na matumizi ya lahaja mbalimbali
  7. Huweza pia kuwa na matumizi ya lugha za kigeni
  8. Huweza pia kufungamanishwa na vipengele vya fasihi simulizi kama vile nahau,methal, lakabu n.k.

See also: