Simba SC Kibaruani na Azam FC Katika Mchezo wa NBC Ligi Kuu | Baada ya ushindi mkubwa dhidi ya Al Ahli Tripoli ya Libya katika mechi ya CAF Confederation Cup, Simba SC inakabiliwa na kibarua kingine kigumu wiki hii. Timu hiyo ya Wekundu wa Msimbazi itakutana na Azam FC katika mechi ya NBC Premier League, ambayo inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Mchezo huu utapigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamanzi, jijini Dar es Salaam, majira ya saa 12:00 jioni.
Azam FC, ambao wameanza msimu huu kwa nguvu, wataingia uwanjani wakitafuta alama tatu muhimu dhidi ya Simba SC, ambao wanakuja na morali ya juu baada ya ushindi wao wa kimataifa. Mechi hii ni ya muhimu kwa timu zote mbili, kwani ushindi unaweza kuimarisha nafasi zao kwenye msimamo wa ligi. Simba SC, ikiwa na lengo la kuendelea kutawala Ligi Kuu ya NBC, itahitaji kuonyesha ubora wake kwenye mchezo huu wa ugenini dhidi ya Azam FC.
Simba SC Kibaruani na Azam FC Katika Mchezo wa NBC Ligi Kuu
Mashabiki wa soka nchini wanatarajia pambano hili kuwa la kuvutia, huku Azam FC ikitumia faida ya kucheza nyumbani, wakati Simba SC watataka kudumisha kasi yao ya ushindi.
ANGALIA PIA:
- Marc-André ter Stegen Kukaa Nje ya Uwanja kwa Miezi Saba Kufuatia Majeraha
- Mpanzu Kutumika Kwenye Michuano ya CAF
- Hawa Hapa Wapinzani wa Simba Kombe la Shirikisho Makundi 2024/25
- Trent Alexander-Arnold Aingia Mazungumzo Kununua Klabu ya FC Nantes
- Tetesi za Usajili Simba SC: Mpanzu Kujiunga na Wekundu wa Msimbazi
Leave a Reply