Takwimu za Pacome Zouzoua Ligi ya Mabingwa Afrika 2023/24

Pacome Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika 2023/24

Takwimu za Pacome Zouzoua Ligi ya Mabingwa Afrika 2023/24 – Wakati Afrika ikibaki na mshangao katika medani za soka kwa kuishuhudia Tanzania kuwa nchi pekee msimu huu kupeleka timu mbili hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mashabiki wa Yanga wanatembea kifua mbele na nyota wao Pacome Zouzoua.

Wananchi wanazo sababu za ‘kujigamba’ na Pacome wao kwa sababu mchezaji huyo ameonesha kiwango bora katika mechi za hatua ya makundi/Takwimu za Pacome Zouzoua Ligi ya Mabingwa Afrika 2023/24.

Katika mechi sita ambazo Yanga imecheza, Pacome ametia kambani magoli matatu. Cheche za ‘mkali huyo wa bleach’ zilianza kuonekana Desemba 2, 2023 kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly. Wakati mashabiki wa Yanga wakiwa kama wamekata tamaa, Pacome akaibuka pasipojulikana na kufunga goli akiwa amezungukwa na wachezaji wa Al Ahly pale Benjmain Mkapa dakika za majeruhi.

Takwimu za Pacome Zouzoua Ligi ya Mabingwa Afrika 2023/24

Takwimu za Pacome Zouzoua Ligi ya Mabingwa Afrika 2023/24

Desemba 8, 2023, Pacome akawainua tena mashabiki wa Yanga ambao tayari walikuwa nyuma kwa goli moja lililofungwa kwa penati na Jonathan Sowah dakika ya 27, Pacome akaibuka tena kusikojulikana na kuwainua Yanga kwa kufunga goli dakika ya 36.

Desemba 20, 2023, Pacome tena akawakosha mashabiki wa Yanga kwa kufunga goli moja kati ya matatu ambayo Wananchi waliyapata dhdi ya Medeama katika dimba la Benjmain Mkapa.

Februari 24, 2024, Pacome Zouzoua hakufunga kwenye ushindi wa Yanga wa magoli 4-0 dhidi ya CR Belouizdad, lakini wapenda soka walikoshwa na burudani aliyoionesha nyota huyo katika dimba la Benjamin Mkapa. Yanga sasa wameanza kuiota nusu fainali. Unatarajia nini kutoka kwa Pacome katika kuwavusha Wananchi kwenda hatua inayofuata?

See also:

Tanzania yapeleka wawakilishi wawili robo fainali ligi ya mabingwa

Ratiba ya Klabu Bingwa Robo fainali 2023/2024 CAF

Matokeo Hatua ya Makundi Klabu Bingwa CAF 2023-2024

Al-Ahly wamemaliza kileleni mwa Kundi A baada ya kushinda 1-0 dhidi ya Young Africans

CAFCL 2023/24: Simba yaungana na Asec Mimosas Robo Fainali

Timu za Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAF 2023/24

Timu aliyopangiwa Yanga CAF 2023/24

Kikosi cha Yanga kinaondoka kuelekea Cairo kumenyana na Ahly

Kikosi Cha Yanga chawasili Cairo, Egypt Kuikabili Al Ahly

Golikipa mwenye clean-sheet nyingi Ligi daraja la kwanza 2023-24

Timu zilizoshinda michezo mingi ya Ligi Daraja la kwanza 2023-24