Tanzania mwenyeji wa mashindano ya Sudan Super League

Tanzania mwenyeji wa mashindano ya Sudan Super League | Taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea barua kutoka kwa Chama cha Mpira wa Miguu nchini Sudan (SFA) wakiomba Tanzania iwe mwenyeji wa mashindano ya Sudan Super League yatakayofanyika kuanzia Juni 25 hadi Juni 30, 2024 katika Azam Complex, Chamazi.

Mashindano haya yanalenga kupeleka ujumbe wa kurudisha amani nchini Sudan. Timu zitakazoshiriki mashindano haya ni:

  • Al-Hilal SC
  • Al-Merrikh
  • Al-Wadi Nyala

Tanzania mwenyeji wa mashindano ya Sudan Super League

Tanzania mwenyeji wa mashindano ya Sudan Super League
Tanzania mwenyeji wa mashindano ya Sudan Super League

Ratiba ya Mechi

Mechi za Super League zitachezwa kuanzia saa 12 jioni. Ratiba ya mashindano ni kama ifuatavyo:

  • 25.06.2024: Al-Hilal SC vs Al-Wadi Nyala
  • 27.06.2024: Al-Wadi Nyala vs Al-Merrikh
  • 30.06.2024: Al-Merrikh vs Al-Hilal SC

Mashindano haya yana umuhimu mkubwa kwani yanaweka mkazo kwenye kurudisha amani nchini Sudan kupitia mchezo wa mpira wa miguu. Timu shiriki zitaonesha umahiri wao huku zikipeleka ujumbe wa umoja na mshikamano kwa watu wa Sudan. Mchezo huo utachezwa katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi, na unatarajiwa kuvutia mashabiki wengi wa mpira wa miguu.

SEE ALSO: