Trent Alexander-Arnold Aingia Mazungumzo Kununua Klabu ya FC Nantes

Trent Alexander-Arnold Aingia Mazungumzo Kununua Klabu ya FC Nantes | Beki wa kulia wa Liverpool, Trent Alexander-Arnold, yuko katika mazungumzo ya kununua klabu ya Ligue 1, FC Nantes, nchini Ufaransa. Mchezaji huyo wa kimataifa wa England, pamoja na kikundi cha uwekezaji, wamewasilisha dau la takriban €100 milioni ili kupata umiliki wa klabu hiyo maarufu.

Hatua hii ni sehemu ya mpango wa Alexander-Arnold kuwekeza katika soka, huku akitazamia kufuata nyayo za wanasoka wengine ambao wameingia katika biashara ya umiliki wa vilabu. Dau hilo la kununua FC Nantes linaashiria azma yake ya kujiimarisha zaidi nje ya uwanja na katika ulimwengu wa biashara.

Trent Alexander-Arnold Aingia Mazungumzo Kununua Klabu ya FC Nantes
Trent Alexander-Arnold Aingia Mazungumzo Kununua Klabu ya FC Nantes

Ikiwa dili hilo litafanikiwa, Trent atakuwa mmoja wa wanasoka wachache wenye umiliki wa klabu katika soka la Ulaya, jambo ambalo linaweza kubadilisha mazingira ya soka na nafasi ya wachezaji kuwa wawekezaji wakubwa.

ANGALIA PIA: