Walimu Kuongeza Ufaulu Kidato cha Nne 2024/2025

Walimu Kuongeza Ufaulu Kidato cha Nne 2024/2025 | Mhe. Mchengerwa Aomba Ongezeko la Ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha nne, walimu wachukue majukumu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa wito kwa walimu wa sekondari wenye ajira ya kudumu na wanaojitolea nchini kufundisha kwa bidii na weledi ili kuunga mkono jitihada za serikali za kuongeza ufaulu wa kidato cha nne.

Mhe. Mchengerwa ametoa wito huo wakati wa kikao kazi chake na walimu wa shule za sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kilichokuwa na lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa walimu hao.

“Walimu ninaomba mkatusaidie kuwapatia elimu bora watoto wetu, na sie upande wa Serikali tutaendelea kuyafanyia kazi mahitaji yenu ili msiwe na kikwazo cha kutekeleza majukumu yenu,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.

Mhe. Mchengerwa amewataka walimu nchini kutumia mbinu na weledi walionao kuwafundisha wanafunzi ili kuongeza ufaulu wa kidato cha nne nchini na kuongeza kuwa, ikiwezekana watumie pia mbinu zilizowawezesha wao kufaulu mpaka wamekuwa walimu wanaotegemewa na taifa.

Walimu Kuongeza Ufaulu Kidato cha Nne 2024/2025
Walimu Kuongeza Ufaulu Kidato cha Nne 2024/2025

Akizungumzia utatuzi wa changamoto ya upatikanaji wa chakula shuleni, Mhe. Mchengerwa amesema Serikali inaendelea kuratibu mpango wa kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni ili waweze kutekeleza jukumu lao la msingi la kupata elimu itakayowawezesha kutoa mchango katika maendeleo ya taifa.

Aidha, amewataka walimu wanaojitolea nchini kuendelea kuchapa kazi kwa bidii kwani mchango wao unahitajika katika kuongeza ufaulu wa kidato cha nne na amewahimiza walimu hao wasisite kuomba ajira pindi Serikali itakapotangaza ajira ili waendelee kulitumikia taifa.

Kikao kazi hicho cha Mhe. Mchengerwa na Walimu kilihudhuriwa pia na Wakuu wa Idara na Vitengo, Watendaji wa Kata, Waratibu wa Elimu Kata, Walimu wa Kujitolea na wasomi wazawa wanaojishughulisha na Elimu waliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji.

ANGALIA PIA: