Waliochaguliwa JKT 2024 watakiwa kuripoti haraka na mapema

Waliochaguliwa JKT 2024 watakiwa kuripoti haraka na mapema, Vijana Waliohitimu Kidato cha Sita 2024 Wakitakiwa Kuripoti Mara Moja Makambi ya JKT: Brigedia Jenerali Hassan Mabena

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limewataka vijana wote waliohitimu kidato cha sita mwaka 2024 na ambao walitakiwa kuripoti makambini kwa ajili ya mafunzo ya lazima kwa mujibu wa sheria kuanzia Juni 1 hadi Juni 7, 2024, lakini bado hawajaripoti, kuhakikisha wanaripoti mara moja kwenye makambi waliyopangiwa wakiwa na vifaa vilivyoainishwa na JKT.

Waliochaguliwa JKT 2024 watakiwa kuripoti haraka na mapema

Maelekezo haya yametolewa na Brigedia Jenerali Hassan Mabena, Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Juni 22, 2024, wakati akitoa taarifa ya nyongeza kwa vijana waliohitimu kidato cha sita mwaka huu kujiunga na mafunzo hayo muhimu. Brigedia Jenerali Mabena amesisitiza kuwa vijana hao wanatakiwa kuripoti kwenye makambi yaliyo karibu nao kuanzia leo Juni 22 hadi Juni 26, 2024.

Waliochaguliwa JKT 2024 watakiwa kuripoti haraka na mapema
Waliochaguliwa JKT 2024 watakiwa kuripoti haraka na mapema

“Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele amewataka vijana waliohitimu kidato cha sita mwaka 2024 kuungana na wenzao ili kujengewa uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia taifa lao,” alisema Brigedia Jenerali Mabena/Waliochaguliwa JKT 2024 watakiwa kuripoti haraka na mapema.

Majukumu na Mafunzo ya JKT kwa Vijana

Jeshi la Kujenga Taifa ni taasisi ya kijamii inayolenga kuwafunza vijana stadi mbalimbali za maisha, kazi, na uzalendo. Mafunzo haya ni ya lazima kwa mujibu wa sheria, na yana lengo la kuwaandaa vijana kuwa raia wema, wenye uwezo wa kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya taifa. Vijana watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yakiwemo stadi za kijeshi, uongozi, na utaalamu wa kazi.

Waliochaguliwa JKT 2024 watakiwa kuripoti haraka na mapema, Kwa vijana wote waliohitimu kidato cha sita mwaka 2024, ni muhimu kutii wito huu na kuripoti mara moja kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa ili kunufaika na mafunzo haya muhimu kwa ajili ya mustakabali mzuri wa taifa letu.

SEE ALSO: