Yamal Aingia kwenye Orodha ya Wachezaji Wenye Umri Mdogo Kufunga UEFA | Lamine Yamal Aweka Rekodi UEFA Champions League kwa Bao la Kwanza Akiwa na Miaka 17
Kinda wa klabu ya FC Barcelona, Lamine Yamal, ameweka rekodi muhimu kwenye soka la Ulaya baada ya kufunga bao lake la kwanza katika michuano ya UEFA Champions League akiwa na umri wa miaka 17, miezi 2, na siku 6. Bao hili linamfanya kuwa mchezaji wa pili mwenye umri mdogo zaidi kufunga bao katika historia ya michuano hiyo, nyuma ya mchezaji mwenzake wa zamani wa Barcelona, Ansu Fati, ambaye alifunga akiwa na miaka 17, mwezi 1, na siku 9.
Yamal Aingia kwenye Orodha ya Wachezaji Wenye Umri Mdogo Kufunga UEFA
Yamal ameonyesha kiwango bora akiwa na umri mdogo sana, akiendelea kuvutia mashabiki wa Barcelona na ulimwengu wa soka kwa ujumla. Orodha ya wachezaji wachanga waliofunga katika UEFA Champions League inaongozwa na:
- Ansu Fati – Miaka 17, Mwezi 1 na Siku 9
- Lamine Yamal – Miaka 17, Miezi 2 na Siku 6
- George Ilenikhena – Miaka 17, Miezi 3 na Siku 27
- Antonio Nusa – Miaka 17, Miezi 4 na Siku 27
Lamine Yamal ameanza kuandika historia yake akiwa na umri mdogo, akiwapa mashabiki wa Barcelona matumaini ya kuwa na mchezaji wa kipekee kwa miaka ijayo.
ANGALIA PIA:
- Matokeo Ya Jana UEFA Champions League 19/09/2024
- Bei ya IPhone 16 Pro Max Tanzania na Zanzibar
- Ratiba ya Raundi ya 2 ya Awali CAF 2024/25
- Feitoto Angia Kwenye Orodha ya Top Assists Ligi Kuu 2024-25
- Azam FC Yaibugiza KMC kwa Ushindi wa 4-0
- FIFA Imechapisha Orodha Mpya za Timu ya Taifa Bora 2024
- Kaizer Chiefs signing new assistant coach for Nabi
Leave a Reply