Yanga Yazitaka Alama 3 kwa Kengold Leo NBC

Yanga Yazitaka Alama 3 kwa Kengold Leo NBC | Matokeo ya mechi ya KenGold dhidi ya Yanga kwenye ligi kuu NBC leo 25/09/2024.

Kocha Gamondi: Yanga Ipo Tayari Kuwakabili Ken Gold, Lengo Ni Pointi Tatu Muhimu

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miguel Gamondi, amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ken Gold, utakaochezwa katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Akizungumzia maandalizi, Gamondi alisisitiza umuhimu wa kupata pointi tatu kwenye mchezo huo, akieleza kuwa ingawa mchezo hautakuwa rahisi, Yanga imejipanga vilivyo.

Yanga Yazitaka Alama 3 kwa Kengold Leo NBC
Yanga Yazitaka Alama 3 kwa Kengold Leo NBC

Hii ni baada ya Yanga kushinda mchezo wao wa kwanza dhidi ya Kagera Sugar kwa mabao 2-0, yaliyofungwa na Clement Mzize na Maxi Nzengeli. Gamondi pia alibainisha kuwa timu yoyote inayokutana na Yanga inakuwa na lengo la kupata matokeo mazuri, hivyo wanacheza kwa tahadhari kubwa.

Ken Gold, timu iliyopanda daraja msimu huu, bado haijapata ushindi katika mechi zake nne za awali za Ligi Kuu msimu wa 2024/25, jambo linalowafanya Yanga kutarajia ushindani wa hali ya juu kutoka kwa wapinzani wao.

ANGALIA PIA: