Rais wa CAF Motsepe Aamuru Uchunguzi, Vurugu Mechi ya Al Ahli Tripol Dhidi ya Simba

Rais wa CAF Motsepe Aamuru Uchunguzi, Vurugu Mechi ya Al Ahli Tripol Dhidi ya Simba — Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), Patrice Motsepe, ameagiza kufanyika uchunguzi wa kina kufuatia vurugu zilizotokea kwenye mechi kati ya Al Ahli Tripoli na Simba SC. Uchunguzi huu umeanzishwa baada ya tukio la machafuko na vurugu kuathiri mchezo huo, hali ambayo imezua maswali kuhusu usalama na haki kwenye mechi za kimataifa.

Mwandishi wa CAF, Collins Okinya, ameripoti kuwa Rais Motsepe ameelezea kushtushwa kwake na hali hiyo na amesisitiza kuwa uchunguzi huo unalenga kuhakikisha haki inatendeka kwa Simba SC. Motsepe amesema ni muhimu klabu kama Simba ipate haki yao kwa mujibu wa taratibu za soka barani Afrika, na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale watakaopatikana na hatia ya kusababisha vurugu hizo.

Rais wa CAF Motsepe Aamuru Uchunguzi, Vurugu Mechi ya Al Ahli Tripol Dhidi ya Simba

Uchunguzi huu unatarajiwa kutoa mwanga juu ya chanzo cha vurugu hizo na namna ya kuhakikisha kwamba matukio kama hayo hayajirudii katika mechi zijazo, hasa katika mashindano ya kimataifa ya CAF.

ANGALIA PIA: