Ratiba ya Mtiani wa Kidato cha Nne 2024

Ratiba ya Mtiani wa Kidato cha Nne 2024 | Taarifa kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania:

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza ratiba ya mtihani wa Taifa kidato cha nne 2024/2025, utakaofanyika kuanzia tarehe 11 Novemba hadi 29 Novemba 2024. Mtihani huu ni muhimu sana katika mfumo wa elimu wa Tanzania, kwani ndio unaotumika kutathmini kiwango cha ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne na kuamua hatua zao zinazofuata katika masomo yao.

Ratiba hii inatoa mwongozo kamili wa tarehe, siku, na muda wa kila somo litakalofanyiwa mtihani. Aidha, inajumuisha maelekezo muhimu kwa wanafunzi, wazazi/walezi, na walimu kuhusu taratibu za mtihani na mambo mengine muhimu yanayohitaji kuzingatiwa.

Mitihani itahusisha masomo ya lazima na ya hiari, ikiwa ni pamoja na Hisabati, Kiingereza, Kiswahili, Jiografia, Fizikia, Kemia, Baiolojia, na mengine mengi. Pia, kutakuwa na mitihani ya vitendo kwa baadhi ya masomo kama vile Baiolojia, Fizikia, na Kemia.

Katika ratiba hii, NECTA imesisitiza kuwa mitihani itaendelea kama ilivyopangwa hata kama siku ya mtihani itaangukia kwenye sikukuu. Aidha, wanafunzi wametakiwa kufika vituoni kwa wakati na kuzingatia maelekezo yote yatakayotolewa na wasimamizi wa mitihani.

Ratiba ya Mtiani wa Kidato cha Nne 2024

Ratiba ya Mtiani wa Kidato cha Nne 2024
Ratiba ya Mtiani wa Kidato cha Nne 2024

Mtihani wa Kidato cha Nne 2024 utafanyika kuanzia tarehe 11/11/2024 hadi 29/11/2024. Pia, Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili utafanyika kuanzia tarehe 28/10/2024 hadi 07/11/2024. Watahiniwa wote wa Kujitegemea waliosajiliwa kufanya mitihani na upimaji huo wanatakiwa kufika katika vituo vyao vya mitihani kwa ajili ya kuchukua barua na kuhakiki taarifa zao.

Vyanzo Rasmi:
Instagram: @necta_tanzania
YouTube: Necta Online
Facebook: NectaTz

ANGALIA PIA: