Tanzania Volleyball National League Kuanza Septemba 27, 2024: Maandalizi Yapo Sawa – Mkurugenzi Rizik Godwin
Ligi ya Taifa ya Wavu Tanzania (Tanzania Volleyball National League) inatarajiwa kuanza rasmi kuanzia Septemba 27 hadi Oktoba 4, 2024 katika viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Utawala wa Shirikisho la Wavu Tanzania, Rizik Godwin, ametoa taarifa juu ya maandalizi ya michuano hiyo, akisema kwamba maandalizi yote yamekamilika kwa asilimia kubwa, huku timu shiriki zikitarajiwa kuonyesha ushindani wa hali ya juu.
Kwa mujibu wa Godwin, mashindano haya yanatarajiwa kuwaleta pamoja timu bora kutoka mikoa mbalimbali nchini, ambapo lengo ni kuimarisha mchezo wa wavu na kuongeza hamasa ya ushiriki wa vijana katika mchezo huo. Pia, Godwin alisisitiza kuwa viwanja vya Mwembe Yanga vimeandaliwa vyema ili kuhakikisha mashindano yanafanyika kwa viwango vya kimataifa, huku usalama wa wachezaji na mashabiki ukipewa kipaumbele.
Mashindano haya ya Ligi ya Taifa ya Wavu yamekuwa sehemu muhimu katika kukuza vipaji vya wachezaji wa ndani na kutoa nafasi kwao kujiandaa kwa mashindano ya kimataifa. Shirikisho la Wavu Tanzania limeweka mikakati thabiti ya kuhakikisha ligi hii inafanikiwa na kutoa hamasa kwa wachezaji na wapenzi wa mchezo huo.
ANGALIA PIA:
Leave a Reply