Azam FC Yaibugiza KMC kwa Ushindi wa 4-0

Azam FC Yaibugiza KMC kwa Ushindi wa 4-0 | Feisal Salum ‘Feitoto’ Aanika Ligi Kuu kwa “Assists” Mbili, Azam FC Yawalaza KMC kwa Ushindi wa 4-0

Kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Feitoto,’ ameanza rasmi kampeni yake ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kiwango cha juu baada ya kutoa pasi mbili za magoli (“assists”) katika ushindi wa 4-0 dhidi ya KMC kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.

Baada ya kuanza ligi kwa matokeo yasiyoridhisha na timu yake kushindwa kufunga katika michezo miwili ya awali, Feisal ameonyesha uwezo wake wa kipekee katika mchezo huu, akiisaidia Azam kupata matokeo muhimu. Magoli ya Azam FC yalifungwa na wachezaji:

Azam FC Yaibugiza KMC kwa Ushindi wa 4-0

Azam FC Yaibugiza KMC kwa Ushindi wa 4-0

  • ⚽ Iddi Bado
  • ⚽ Lusajo Mwaikenda
  • ⚽ Nassor Saadun
  • ⚽ Nathaniel Chilambo

Ushindi huu mnono unawaweka Azam FC kwenye nafasi nzuri ya kurudi kwenye ushindani wa ligi, huku mchango wa Feisal Salum ukiwa kiini cha mafanikio yao katika mchezo huu.

ANGALIA PIA: