CAF Super Cup 2024 Fainali, Al Ahly vs Zamalek

CAF Super Cup 2024 Fainali, Al Ahly vs Zamalek | Leo usiku, macho na masikio ya mashabiki wa soka barani Afrika yataelekezwa kwenye uwanja wa Kingdom Arena, ambapo utachezwa mchezo wa kusisimua wa CAF Super Cup 2024. Hii ni mechi inayowakutanisha vigogo wawili wa soka kutoka Misri – Al Ahly, mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika 2024, dhidi ya Zamalek, ambao ni mabingwa wa Kombe la Shirikisho la Afrika 2024.

Mtanange huu utapigwa kuanzia saa 3:00 usiku na utarushwa moja kwa moja kupitia Azam Sports 2 HD. Mashabiki wana matumaini makubwa ya kushuhudia mchezo wa kiwango cha juu, kwani timu zote mbili zina historia ndefu na yenye mafanikio katika soka la Afrika.

CAF Super Cup 2024 Fainali, Al Ahly vs Zamalek
CAF Super Cup 2024 Fainali, Al Ahly vs Zamalek

Al Ahly, maarufu kwa kutawala michuano ya kimataifa, wanatazamia kuongeza taji jingine la Super Cup kwenye kabati lao la mataji. Wakati huo huo, Zamalek hawatakuwa tayari kuruhusu wapinzani wao wa jadi kuwazidi kete, wakiwa na njaa ya ushindi katika fainali hii.

Je, ni Al Ahly wataendelea kuandika historia yao kama klabu yenye mafanikio zaidi barani Afrika, au ni Zamalek watakaoweka heshima kwa kuchukua kombe hili na kumaliza ukame wao wa Super Cup? Hili ni swali ambalo litapata jibu usiku wa leo. Mchezo huu si wa kukosa kwa mashabiki wa soka wa bara zima!

ANGALIA PIA: