FIFA Yaamuru Yanga SC Kumlipa Augustine Okrah Milioni 820

FIFA Yaamuru Yanga SC Kumlipa Augustine Okrah Milioni 820

FIFA Yaamuru Yanga SC Kumlipa Augustine Okrah Milioni 820 | Kamati ya Usuluhishi ya FIFA imeiamuru klabu ya Young Africans SC (Yanga) kumlipa kiasi cha takribani shilingi milioni 820 kwa mchezaji wa zamani Augustine Okrah, ikiwa ni malipo ya fidia baada ya klabu hiyo kuvunja mkataba wake. Uamuzi huu umetolewa baada ya mchezaji huyo kufungua shauri dhidi ya Yanga kufuatia mkataba wake kuvunjwa kinyume na taratibu.

Kwa mujibu wa uamuzi wa FIFA, Yanga wanatakiwa kumlipa Okrah ndani ya kipindi cha siku 45. Iwapo mabingwa hao wa Tanzania watashindwa kumlipa mchezaji huyo katika muda uliowekwa, wapo hatarini kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu. Mojawapo ya adhabu hizo ni kufungiwa kufanya usajili kwa madirisha matatu mfululizo, jambo ambalo linaweza kuwa pigo kubwa kwa klabu hiyo yenye malengo makubwa ya kimataifa.

FIFA Yaamuru Yanga SC Kumlipa Augustine Okrah Milioni 820
FIFA Yaamuru Yanga SC Kumlipa Augustine Okrah Milioni 820

Okrah, ambaye alijiunga na Yanga na kuonyesha kiwango kizuri katika michuano ya ndani na nje ya nchi, anaamini kuwa haki yake imetendeka kupitia uamuzi huu wa FIFA. Yanga, kwa upande wao, wanakabiliwa na changamoto ya kuhakikisha wanatekeleza uamuzi huo ili kuepuka vikwazo vinavyoweza kudhoofisha mipango yao ya baadaye.

Sasa ni suala la muda tu kuona kama Yanga watakamilisha malipo hayo ndani ya siku 45 au watakabiliwa na athari za kutozingatia agizo hilo la FIFA.

ANGALIA PIA: