Kikosi cha Taifa Stars Kilichoitwa kwa Michezo Dhidi ya Ethiopia na Guinea

Kikosi cha Taifa Stars Kilichoitwa kwa Michezo Dhidi ya Ethiopia na Guinea | Kocha Hemed Suleiman Atangaza Kikosi cha Taifa Stars kwa Michezo ya Kufuzu AFCON 2025 Dhidi ya Ethiopia na Guinea

Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Hemed Suleiman, leo ametangaza kikosi kitakachoshiriki michezo miwili muhimu ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 dhidi ya Ethiopia na Guinea. Kikosi hiki kinajumuisha wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi pamoja na wale wa ligi ya ndani, hatua ambayo inalenga kuleta uwiano wa uzoefu na vipaji vya ndani.

Katika mkakati huu wa kufuzu, kocha Suleiman ameongeza baadhi ya wachezaji wenye uzoefu wa mashindano ya kimataifa, ambao hawakupata nafasi kwenye kikosi kilichopita. Huu ni muendelezo wa juhudi za Taifa Stars kuimarisha timu kwa ajili ya kuhakikisha inapata matokeo mazuri katika mechi hizi mbili muhimu.

Kikosi cha Taifa Stars Kilichoitwa kwa Michezo Dhidi ya Ethiopia na Guinea

Kifuatacho ni kikosi cha wachezaji wa Tanzania Taifa Stars watakaowakilisha taifa kwenye michezo ya kufuzu AFCON 2025 dhidi ya Guinea na Ethiopia mwezi huu novemba:-

Kikosi cha Taifa Stars Kilichoitwa kwa Michezo Dhidi ya Ethiopia na Guinea
Kikosi cha Taifa Stars Kilichoitwa kwa Michezo Dhidi ya Ethiopia na Guinea

KIKOSI CHA TAIFA STARS KITAKACHOINGIA KAMBINI KUJIANDAA NA MICHEZO MIWILI YA KUFUZU AFCON 2025 DHIDI YA ETHIOPIA NA GUINEA

  1. Aishi Manula (Simba SC)
  2. Zuberi Foba (Azam FC)
  3. Metacha Mnata (Singida Black Stars)
  4. Lusajo Mwaikenda (Azam FC)
  5. Shomari Kapombe (Simba SC)
  6. Mohamed Hussein (Simba SC)
  7. Paschal Msindo (Azam FC)
  8. David Bryson (JKT Tanzania)
  9. Ibrahim Hamad (Young Africans)
  10. Dickson Job (Young Africans)
  11. Muhamed Ame (Mashujaa FC)
  12. Abdulrazack Hamza (Simba SC)
  13. Adolf Mtsinzigwa (Azam FC)
  14. Novatus Dismas (Goztepe, Uturuki)
  15. Habib Khalid (Singida Black Stars)
  16. Mudathir Yahya (Young Africans)
  17. Feisal Salum (Azam FC)
  18. Mbwana Samatta (PAOK FC, Ugiriki)
  19. Clement Mzize (Young Africans)
  20. Kibu Dennis (Simba SC)
  21. Simon Msuva (Al-Talaba, Iraq)
  22. Idd Nado (Azam FC)
  23. Ismail Mgunda (Mashujaa FC)
  24. Abdulkarim Ally Pius Kichuya (Azam FC U20)
  25. Cyprian Kachwele (Vancouver Whitecaps, Canada)
  26. Nasoro Saadun (Azam FC)

Kocha: Hemed Suleiman

Ni ishara kuwa Taifa Stars inakwenda katika michezo hiyo ikiwa na nguvu mpya, na hari ya kutafuta matokeo mazuri kwenye michezo hii licha ya ushindani uliopo kwenye kundi hili.

ANGALIA PIA: