Marc-André ter Stegen Kukaa Nje ya Uwanja kwa Miezi Saba Kufuatia Majeraha

Marc-André ter Stegen Kukaa Nje ya Uwanja kwa Miezi Saba Kufuatia Majeraha | Kipa wa Barcelona, Marc-André ter Stegen, anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi saba kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata katika goti lake la kulia. Kipa huyo wa kimataifa wa Ujerumani aliumia wakati wa pambano la La Liga kati ya Barcelona na Villarreal, na baada ya vipimo, imebainika kuwa anahitaji kufanyiwa upasuaji wa dharura.

Taarifa rasmi iliyotolewa na klabu ya Barcelona imethibitisha kuwa Ter Stegen atafanyiwa upasuaji huo leo, na baada ya hapo atahitajika kupumzika kwa muda wa miezi saba ili kuhakikisha anapata nafuu kamili. Majeraha haya yanakuja katika kipindi ambacho Barcelona inakabiliana na mashindano mbalimbali, yakiwemo La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya, hivyo kutokuwepo kwake kutakuwa pigo kubwa kwa timu hiyo.

Marc-André ter Stegen Kukaa Nje ya Uwanja kwa Miezi Saba Kufuatia Majeraha
Marc-André ter Stegen Kukaa Nje ya Uwanja kwa Miezi Saba Kufuatia Majeraha

Ter Stegen amekuwa ni mchezaji muhimu katika kikosi cha Barcelona, akijulikana kwa umahiri wake wa kulinda lango na uwezo wa kusambaza mipira kwa usahihi. Kuumia kwake kunawapa changamoto kubwa Barcelona, ambao sasa watakuwa wakitegemea kipa mbadala kushika nafasi yake katika michezo ijayo.

Huku upasuaji ukipangwa kufanyika haraka, mashabiki na wachezaji wa Barcelona wanatarajia kumwona Ter Stegen akipona haraka na kurejea tena uwanjani akiwa na nguvu zake za awali/Marc-André ter Stegen Kukaa Nje ya Uwanja kwa Miezi Saba Kufuatia Majeraha.

ANGALIA PIA: