Mashujaa FC Yaendeleza Wimbi la Ushindi, Yatinga Nafasi ya Pili

LIGI KUU TANZANIA BARA | Mashujaa FC Yaendeleza Wimbi la Ushindi, Yatinga Nafasi ya Pili.

Mashujaa FC imeendelea kuonesha ubora wake baada ya kushinda mchezo wa pili mfululizo kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, safari hii wakiibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal Union. Goli la pekee katika mchezo huo lilifungwa na Gushi kipindi cha kwanza, ambalo liliipa Mashujaa FC alama zote tatu muhimu.

Kwa matokeo haya, Mashujaa FC imejipatia alama 7, baada ya kushinda mechi mbili na kutoa sare moja, na hivyo kujikita kwenye nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

Mashujaa FC Yaendeleza Wimbi la Ushindi, Yatinga Nafasi ya Pili
Mashujaa FC Yaendeleza Wimbi la Ushindi, Yatinga Nafasi ya Pili

Kwa upande wa Coastal Union, hali inaonekana kuwa ngumu baada ya kukosa alama kwa mara ya pili mfululizo, jambo ambalo linaweza kuleta changamoto kwao kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi msimu huu.

Matokeo ya Mwisho:
Coastal Union 0-1 Mashujaa FC

ANGALIA PIA: