MATOKEO Team Kibwana 2-6 Team Job Mechi ya Hisani

MATOKEO Team Kibwana 2-6 Team Job Mechi ya Hisani | Baada ya tambo nyingi hatimae kimefaamika nani mbabe wa mwenzie kwenye mchezo uliochezwa na Team Kibwana dhidi ya Team Job ambapo Team Kibwana imegaragazwa vibaya kwa kichapo cha magoli 6 kwa 2 kwenye mchezo uliochezwa leo majira ya saa kumi kamili katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Team Job imepata ushindi wa magoli 6 kupitia wachezaji wake Eris Said aliefunga goli la utangulizi dakika ya 14, goli la pili likafungwa na Ndemla dakika ya 24 akipiga shuti mmenyo nje ya box, goli la tatu lili fungwa na ‘mtoto wa mfalme’ Dube kwa mpira wa hazabu ndogo ulipigwa na Ndemla na kuonganishwa kwa kichwa na Dube dakika ya 26.

Goli la nne lilifungwa na Mpole Gorge dakika ya 70 akipokea pasi zuri kutoka kwa Mzize, Goli la Tano lilifungwa na Mbangula dakika ya 78 ya mchezwa na goli la kufungia kurasa ya magoli lilifungwa na Balua Edwin dakika ya 90’+3 ya mchezo.

MATOKEO Team Kibwana 2-6 Team Job Mechi ya Hisani
MATOKEO Team Kibwana 2-6 Team Job Mechi ya Hisani

Magoli ya Team Kibwana yamefungwa na Msuva kwa free-kick ya viwango kabisa dakika ya 30 ya mchezo likiwa ndo goli la kwanza na gpoli la pili likafungwa na Msuva kwa penati (Panenka) ya viwango kabisa dakika ya 47 ya mchezo na Matokeo kutamatika kwa goli 2 kwa 6.

MATOKEO Team Kibwana 2-6 Team Job Mechi ya Hisani

SEE ALSO: