NAFASI za Kazi 8900 za Wahudumu wa Afya

NAFASI za Kazi 8900 za Wahudumu wa Afya: TANGAZO LA NAFASI ZA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII 8,900. Serikali imetangaza nafasi za kazi kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii 8,900 watakaokwenda kutekeleza afua jumuishi za afya, lishe na ustawi wa jamii katika ngazi ya vitongoji na vijiji.

Tangazo lililotolewa leo Jumamosi Aprili 6, 2024 na Wizara ya Afya kwa ushirikiano na Ofisi ya Rais Tamisemi limeeleza kuwa hivi sasa Serikali inatekeleza mpango jumuishi wa wahudumu wa afya wa ngazi ya jamii nchini.

Kupitia mpango huo, Serikali imeweka utaratibu wa kuwapata wahudumu wenye sifa zilizowekwa kutoa mafunzo na kuwatumia wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika utekelezaji wa afua hizo. Mpango huo unahitaji wahudumu wawili mwanamke na mwanaume.

NAFASI za Kazi 8900 za Wahudumu wa Afya

NAFASI za Kazi 8900 za Wahudumu wa Afya

Kwa mujibu wa tangazo hilo, awamu ya kwanza ya mpango huo utaanza kwenye mikoa 10 na halmashauri mbili kwa kila mkoa na itakayonufaika ni Geita wahudumu 920, Kagera (878), Kigoma (1094), Lindi (1724), Mbeya (836), Njombe (746), Pwani (480), Songwe (774), Tabora (966) na Tanga (482).

See also: