Ratiba Ngao ya Jamii Wanawake 2024

Ratiba Ngao ya Jamii Wanawake 2024 | Ngao ya Jamii kwa Wanawake Kufanyika Septemba 24-27 Jijini Dar es Salaam

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuwa michuano ya Ngao ya Jamii kwa upande wa Wanawake, inayoashiria ufunguzi rasmi wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake, itafanyika kuanzia Septemba 24 hadi 27 katika uwanja wa Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Timu nne zinazoshiriki ni Simba Queens, mabingwa watetezi wa ligi, JKT Queens, Yanga Princess, na Ceasiaa Queens. Mashabiki wanatarajia kushuhudia mechi za kusisimua, ikiwemo dabi kubwa kati ya Simba Queens na Yanga Princess kwenye hatua ya Nusu Fainali. Wakati huo huo, JKT Queens watakutana na Ceasiaa Queens katika pambano lingine la Nusu Fainali.

Ratiba Ngao ya Jamii Wanawake 2024

Ratiba ya michuano ya Ngao ya Jamii kwa Wanawake 2024, Mechi hizi zitafanyika kuanzia tarehe 24 Septemba 2024 hadi 27 Septemba 2024 katika uwanja wa KMC Stadium – Mwenge, jijini Dar es Salaam.

Ratiba Ngao ya Jamii Wanawake 2024
Ratiba Ngao ya Jamii Wanawake 2024

Ratiba ya Nusu Fainali:

  1. 24/09/2024 – Saa 13:00:
    JKT Queens vs Ceasiaa Queens
  2. 24/09/2024 – Saa 16:00:
    Simba Queens vs Yanga Princess

Mechi za Kucheza Nafasi ya Tatu na Fainali:

  1. 27/09/2024 – Saa 13:00:
    Timu zitakazopoteza Nusu Fainali (Loser SF1 vs Loser SF2)
  2. 27/09/2024 – Saa 16:00:
    Timu zitakazoshinda Nusu Fainali (Winner SF1 vs Winner SF2)

Michuano hii ni muhimu kwa kuashiria mwanzo wa msimu mpya na kutoa taswira ya hali ya ushindani itakayokuwepo katika ligi kuu ya Wanawake msimu huu/Ratiba Ngao ya Jamii Wanawake 2024.

ANGALIA PIA: