Simba Queens na Yanga Princess Ngao ya Jamii 2024

Simba Queens na Yanga Princess Ngao ya Jamii 2024 | Simba Queens Kucheza na Yanga Princess Katika Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii

Ratiba ya Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii kwa timu za Wanawake imetangazwa, ambapo Simba Queens itakutana na Yanga Princess katika mechi ya Nusu Fainali ya pili. Michuano ya Ngao ya Jamii inahusisha timu nne bora na ni kiashiria cha kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake 2024/25.

Mchezo huu wa kusisimua utapigwa Jumanne, Septemba 24, saa 10:00 jioni, katika Uwanja wa KMC Complex. Mshindi wa pambano hili atatinga fainali na kukutana na mshindi kati ya JKT Queens na Ceasia Queens, ambao watacheza fainali tarehe 27 Septemba 2024 katika uwanja huo huo wa KMC Complex.

Simba Queens na Yanga Princess Ngao ya Jamii 2024
Simba Queens na Yanga Princess Ngao ya Jamii 2024

Kikosi cha Simba Queens kinaendelea na mazoezi chini ya kocha Mussa Hassan Mgosi, kikiwa na lengo thabiti la kutetea taji hili, ambalo Simba Queens ndio mabingwa watetezi. Mashabiki wanatarajia kuona burudani ya hali ya juu na ushindani mkali katika michuano hii.

ANGALIA PIA: