Simba Wawasili Zanzibar kwaajili ya Mzizima Derby Dhidi ya Azam

Simba Wawasili Zanzibar kwaajili ya Mzizima Derby Dhidi ya Azam

Simba Wawasili Zanzibar kwaajili ya Mzizima Derby Dhidi ya Azam | Simba SC Dhidi ya Azam FC Septemba 26, 2024

Klabu ya Simba SC imewasili Zanzibar leo kwa maandalizi ya mchezo mkubwa wa Mzizima Derby dhidi ya Azam FC, utakaofanyika tarehe 26 Septemba 2024 katika Uwanja wa New Amaan Complex. Derby hii ya kihistoria kati ya timu hizi mbili kutoka Dar es Salaam inatarajiwa kuwa moja ya michezo yenye ushindani mkali zaidi msimu huu wa Ligi Kuu ya NBC.

Simba SC, wakiwa na morali ya ushindi kutoka michezo yao ya awali, watalazimika kujituma vilivyo dhidi ya Azam FC ambao pia wapo katika kiwango bora. Mashabiki wa soka kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wanatarajia burudani kali, huku kila timu ikilenga kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi.

Simba Wawasili Zanzibar kwaajili ya Mzizima Derby Dhidi ya Azam
Simba Wawasili Zanzibar kwaajili ya Mzizima Derby Dhidi ya Azam

Mzizima Derby imekuwa ni moja ya mechi zinazovutia hisia za mashabiki wa soka nchini, na mechi ya mwaka huu inatarajiwa kuwa na mvuto wa kipekee, ikizingatiwa ukubwa wa majina ya timu zinazoshiriki.

ANGALIA PIA: