Szczesny Athibitisha Mazungumzo ya Kuhamia Barcelona

Szczesny Athibitisha Mazungumzo ya Kuhamia Barcelona

Szczesny Athibitisha Mazungumzo ya Kuhamia Barcelona | Wojciech Szczesny Athibitisha Kujiunga na Barcelona kama Mazungumzo yatakuwa sawa

Wojciech Szczesny, kipa wa Juventus na timu ya taifa ya Poland, amethibitisha kwamba yupo kwenye mazungumzo ya kujiunga na klabu ya FC Barcelona kama wakala huru. Akizungumza na Sport, Szczesny alieleza kwamba Barcelona ni moja ya klabu bora duniani, na anazingatia kwa umakini fursa ya kujiunga nao. Aliongeza kuwa kutofikiria chaguo hilo ingekuwa kukosa heshima kwa klabu kama Barcelona.

Szczesny Athibitisha Mazungumzo ya Kuhamia Barcelona

Mazungumzo hayo yanaendelea kufuatia taarifa za jeraha alilopata kipa namba moja wa Barcelona mwishoni mwa wiki, katika mchezo dhidi ya Villarreal. Barcelona inahitaji kujaza nafasi hiyo haraka ili kuhakikisha wanabaki na kipa imara kwa michuano inayokuja. Szczesny, akiwa na uzoefu mkubwa kwenye soka la kimataifa, anaweza kuwa chaguo sahihi kwa Barcelona katika kipindi hiki kigumu.

ANGALIA PIA: