Timu zinazoshiriki CECAFA Kagame Cup 2024

Timu zinazoshiriki CECAFA Kagame Cup 2024, Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), limetangaza kwamba mashindano ya Cecafa Kagame Cup mwaka 2024 yatafanyika Tanzania Bara na Zanzibar kuanzia Julai 6 hadi 22 mwaka huu.

Katika taarifa yao ya awali iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa CECAFA, John Auko Gecheo, ilionyesha timu shiriki zitakuwa 16 huku tatu zikiwa ni mwalikwa na 13 zinatokea Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Timu tatu mwalikwa ni TP Mazembe (DR Congo), Nyasa Big Bullets (Malawi) na Red Arrows FC ya Zambia.

Awali, mashindano hayo yalipangwa kufanyika kuanzia Julai 20 hadi Agosti 4 mwaka huu nchini Tanzania, lakini kutokana na ratiba ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuonyesha kuanza Agosti mashindano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho yanaanza, Cecafa limeona mashindano yao yaanze mapema na kumalizika siku chache kabla ya kuanza kwa mtifuano wa michuano ya CAF ngazi ya klabu msimu wa 2024/2025.

Timu zinazoshiriki CECAFA Kagame Cup 2024, Michuano hiyo imerejea baada ya kutofanyika kwa miaka miwili tangu mara ya mwisho iliposhuhudiwa Express ya Uganda ikiwa bingwa mwaka 2021.

Timu zinazoshiriki CECAFA Kagame Cup 2024

Ukiachana na timu tatu zilizoalikwa ambazo zimeainishwa hapo juu huku Simba, Yanga, Azam na JKU zikibaki kwenye sintofahamu, zingine kutoka Ukanda wa Cecafa zitakazoshiriki kwa mujibu wa CECAFA ni Vital’O (Burundi), APR (Rwanda), El Merreikh, Al Hilal, Hai El Wadi (Sudan), Gor Mahia (Kenya), SC Villa (Uganda), El Merreikh FC-Bentiu (Sudan Kusini), Nyasa Big Bullets (Malawi), TP Mazembe (DR Congo), Red Arrows (Zambia) na Coastal Union (Tanzania).

Timu zinazoshiriki CECAFA Kagame Cup 2024
Timu zinazoshiriki CECAFA Kagame Cup 2024

FEDHA ZA WASHINDI/Zawadi za mshindi wa Kagame Cup 2024

Mpaka sasa mashindano hayo bado yamebeba jina la Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kutokana na ufadhili wake mbalimbali anaotoa ikiwemo fedha za zawadi kwa washindi (Dola za Marekani 60,000) ambapo mshindi anapata Dola za Marekani 30,000, atakayeshika nafasi ya pili anazawadiwa Dola za Marekani 20,000 na yule wa tatu Dola za Marekani 10,000.

Mbali na zawadi hizo, Rais Kagame pia anatoa Dola za Marekani 15,000 kila mwaka kwa maandalizi ya michuano hiyo na kufanya mchango wake jumla kuwa dola 75,000.

Historia ya MABINGWA

Simba SC ndio mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo baada ya kushinda mara sita katika miaka ya 1974, 1991, 1992, 1995, 1996 na 2002, ikifuatiwa na Gor Mahia ya Kenya iliyoshinda mara tano katika miaka ya 1979, 1982, 1983, 1984 na 1997.

Yanga ya Tanzania nayo imeshinda taji hilo mara tano katika miaka ya 1975, 1993, 1999, 2011 na 2012 sawa na Tusker, zamani Breweries ya Kenya katika miaka ya 1988, 1989, 2000, 2001 na 2008.

See Also: