Namungo Yashinda Mchezo wa Kwanza Ligi Kuu vs Coastal

Namungo Yashinda Mchezo wa Kwanza Ligi Kuu vs Coastal | Baada ya michezo mitatu mfululizo kupoteza leo Namungo dhidi ya Coastal Union imepata ushindi.

Namungo ilikuwa miongoni mwa timu chache Ligi Kuu ambazo azikuwai pata ushindi kwenye mchezo wao wa ligi kuu, hatimae leo kwenye mchezo dhidi ya coastal Union wameubuka na ushindi wa magoli 2-0 magoli yaliyo fungwa na Rich Koli dakika ya 38′ na dakika za mwisho za kipindi cha kwanza Pius Buswita (45’+2) kuwapa uongozi wa goli mbili.

Kipindi cha pili akikushuhudia goli lolote lica ya mpira kuwa wa kasi na kila timu kutengeneza nafasi bila kunufaika nazo. Hadi dakika 90′ kutamatika na kushuhudia Namungo kupata alama tatu za kwanza kwenye ligi kuu msimu huu wa 2024/2025.

Namungo Yashinda Mchezo wa Kwanza Ligi Kuu vs Coastal
Namungo Yashinda Mchezo wa Kwanza Ligi Kuu vs Coastal

Hushindi huu unamaana kubwa sana kwa Namungo, kutokana na kilichokuwa kikisemwa juu ya mustakabali wa kocha wao. Sasa wanatoka kwenye nafasi waliokuwa nayo hawali na kufika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi ya NBC.

Sasa matumaini ya Namungo kurejesha makali yake yamerudi tena na wanaweza kuwa kwenye mwenendo mzuri wa mechi zilizobaki kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara NBC kwa msimu huu.

Matokeo ya Mwisho ya mchezo ni Coastal Union 0-2 Namungo FC

ANGALIA PIA: