Raphael Varane Atangaza Kustaafu Soka Akiwa na Miaka 31

Raphael Varane Atangaza Kustaafu Soka Akiwa na Miaka 31

Raphael Varane Atangaza Kustaafu Soka Akiwa na Miaka 31: kutokana na Majeraha

Raphael Varane, aliyekuwa mlinzi wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, ametangaza rasmi kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 31 kutokana na majeraha yaliyomkabili. Varane alifikia uamuzi huo baada ya muda mrefu wa kupambana na changamoto za kiafya.

Baada ya kuondoka Manchester United, Varane alijiunga na klabu ya Como inayoshiriki ligi ya Italia, lakini kwa sasa anajadiliana na klabu hiyo kuhusu kusitisha mkataba wake. Katika maisha yake ya soka, Varane amecheza jumla ya mechi 573, akifunga mabao 26 na kutoa pasi za mabao 8.

Raphael Varane Atangaza Kustaafu Soka Akiwa na Miaka 31

Varane atakumbukwa kwa mafanikio makubwa, ikiwa ni pamoja na kushinda mataji ya UEFA Champions League akiwa na Real Madrid, pamoja na Kombe la Dunia la 2018 akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa. Uamuzi wake wa kustaafu mapema kutokana na majeraha umeshtua mashabiki wengi wa soka kote duniani.

ANGALIA PIA: